• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ligi Kuu Uingereza (EPL), Hatimaye Manchester City Bingwa

  (GMT+08:00) 2019-05-13 10:07:26

  Wahenga husema usiku wa deni haukawii kukucha, kikosi cha klabu ya Manchester City ndio mabingwa kwa mara ya pili mfululizo wa ligi kuu ya Uingereza (EPL) msimu wa 2018/19 baada ya jana kuwachapa Brighton & Hove Albion goli 4-1 uwanjani Amex Falmer East Sussex katika mchezo wa mwisho wa msimu.

  Man City imemaliza ligi kwa kunyakua alama 98 moja zaidi ya Liverpool waliomaliza nafasi ya pili ambapo jana nao waliwachabanga Wolverhampton Wanderers magoli2-0, huku Chelsea imekamata nafasi ya tatu imelazimishwa suluhu ya 0-0 dhidi ya Leicester City.

  Tottenham imeambulia nafasi ya nne katika msimamo wa ligi hiyo baada ya kumaliza msimu kwa sare ya goli 2-2 na Everton. Manchester United imeangukia pua baada ya kukubali kipigo cha 2-0 toka kwa Cardiff City, Newcastle United imeicharaza Fulham goli 4-0.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako