• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China ahimiza mazungumzo ya ustaarabu ya Asia

  (GMT+08:00) 2019-05-13 18:39:27

  Miaka mitano iliyopita, rais Xi Jinping wa China alipendekeza kufanyika kwa mazungumzo ya ustaarabu ya Asia, na tarehe 15 pendekezo hilo litatimizwa. Wajumbe kutoka nchi 47 za Asia pamoja na wasomi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa watakutana hapa Beijing, na kufanya mazungumzo yenye kauli mbiu ya "kuwasiliana na kuigana katika mambo ya ustaarabu, na jumuiya yenye hatma ya pamoja".

  "Ua moja sio ishara ya majira ya mchipuko, bali ni maua mengi yanayochunua kwenye bustani". Rais Xi Jinping wa China mwezi Machi mwaka 2014 alipohutubia kikao cha Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, alinukuu shairi la kichina ili kufafanua mawazo yake kuhusu uanuai wa ustaarabu. Anasema,

  "Tunahitaji mawazo mapana katika kuutendea ustaarabu mwingine. Tunapaswa kuhimiza ustaarabu tofauti kuheshimiana na kuwepo pamoja kwa amani, na kuyafanya mawasiliano ya ustaarabu yawe daraja la urafiki kati ya watu wa nchi tofauti, injini ya maendeleo ya jamii ya binadamu, na nguvu ya kudumisha amani ya dunia. Aidha, tunapaswa kutafuta busara kutoka kwenye ustaarabu mbalimbali, ili kukabiliana na changamoto za pamoja za binadamu."

  Katika miaka kadhaa iliyopita, rais Xi alifafanua mara nyingi mawazo ya China kuhusu ustaarabu, ambayo yamekubaliwa na jumuiya ya kimataifa. Aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa Bi. Irina Bokova anasema,

  "Miaka mitano iliyopita, kwa fahari kubwa nilimpokea rais Xi kwenye makao makuu ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni. Alifafanua mawazo yake kuhusu China na mustakabali wa dunia, na maoni kuhusu mawasiliano ya ustaarabu tofauti. Naona hii ilikuwa ishara yenye nguvu kubwa kwa dunia, na ni mawazo na utafiti kuhusu maisha, harakati na maendeleo ya pamoja ya binadamu wote."

  Asia ni bara lenye karibu asilimia 70 ya watu, na theluthi moja ya uchumi wa dunia, na pia lina anuwai kubwa ya ustaarabu. Kwenye Mkutano wa Kilele wa Ushirikiano na Uaminifu wa Asia uliofanyika mjini Shanghai mwaka 2014, na mkutano wa mwaka 2015 wa Baraza la Asia la Bo'ao, rais Xi alipendekeza mara mbili kuitisha mazungumzo ya ustaarabu ya Asia. Anasema,

  "Inapaswa kuhimiza mawasiliano na mazungumzo kati ya ustaarabu na mifumo tofauti ya maendeleo, ili kupata maendeleo ya pamoja. China inapendekeza kufanya mazungumzo ya ustaarabu ya Asia, yanayolenga kuongeza maudhui ya maisha ya kiakili ya watu, na uhai wa ushirikiano wa kimaendeleo barani Asia, kupitia kuhimiza mawasiliano ya vijana, mashirika ya umma, serikali za mitaa na vyombo vya habari, na kuunda mtandao wa mawasiliano na ushirikiano wa washauri mabingwa."

  Mazungumzo ya Ustaarabu ya Asia yatafanyika tarehe 15 mjini Beijing, na kuwashirikisha zaidi ya wajumbe 2,000 kutoka nchi 47 za Asia pamoja na nchi nyingine na mashirika ya kimataifa. Ofisa mwandamizi wa tume ya maandalizi ya mazungumzo hayo Bw. Xu Lin anasema,

  "Madhumuni ya kuandaa mazungumzo hayo ni kurithi na kueneza vizuri zaidi matokeo ya ustaarabu wa nchi za Asia na dunia nzima, na kuhimiza mawasiliano na maelewano kati ya nchi zenye ustaarabu tofauti, ili kuhimiza maendeleo ya ustaarabu wa binadamu, na kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako