• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kaberia aongoza maafisa wa michezo ya Olimpiki wa Kenya katika ziara nchini Japan

    (GMT+08:00) 2019-05-14 09:02:37
    Katibu mkuu wa michezo ya Olimpiki nchini Kenya Kirimi Kaberia akiambatana na maafisa wa kamati ya Olimpiki na riadha ya Kenya wamewasili Japan kwa ajili ya ziara ya mafunzo.

    Kaimu Katibu mkuu wa kamati ya Olimpiki ya Kenya Francis Mutuku amewaambia waandishi wa habari kuwa maafisa hao leo jumanne watakutana na Meya wa mji wa Yokohama na baadaye watatembelea kiwanja kipya cha mpira wa wavu. Kenya na Japan zilisaini ushirikiano ambao utawezesha timu ya Olimpiki ya Kenya kupiga kambi katika kisiwa cha Kyushu jimbo la Fukuoka kujiandaa kwa mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika Tokyo Japan mwakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako