• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bei za hisa katika Soko la hisa la New York zaporomoka kutokana na mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani

  (GMT+08:00) 2019-05-14 10:39:18

  Bei za hisa katika Soko la hisa la New York nchini Marekani zimeporomoka kutokana na kupamba moto kwa mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani.

  Wiki iliyopita serikali ya Marekani ilitangaza ghafla kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China zenye thamani ya dola bilioni 200 za kimarekani kutoka asilimia 10 hadi asilimia 25 kuanzia Mei 10. Jumatatu wiki hii kamati ya ushuru ya Baraza la serikali la China pia ilitangaza kuinua viwango vya ushuru dhidi ya baadhi ya bidhaa za Marekani, ikiwa ni jibu kwa hatua ya Marekani.

  Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na Benki ya Goldman Sachs ya Marekani imesema utafiti umeonesha kuwa ni makampuni na wateja wa Marekani wanaolipa gharama zote zinazotokana na hatua ya Marekani ya kutoza ushuru mkubwa dhidi ya bidhaa za China. Ripoti pia imesema kama mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani ukiendelea kupamba moto, utapunguza ongezeko la GDP la Marekani kwa asilimia 0.4 na zaidi.

  Kamati ya ushuru ya Baraza la serikali la China imesema kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za Marekani kunalenga kujibu sera za Marekani za upande mmoja na kujilinda kibiashara. Pia imesema inatumai kuwa Marekani itarejea kwenye njia sahihi ya mazungumzo, kushirikiana na kwenda sambamba na China, ili pande hizo mbili ziweze kufikia makubaliano ya kunufaishana kwenye msingi wa kuheshimiana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako