• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Skinner wa Marekani ahimizwa kutopaka matope ustaarabu

  (GMT+08:00) 2019-05-14 16:45:09

  Mkurugenzi wa ofisi ya mambo ya mipango ya sera ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani Bibi Kiron Skinner hivi karibuni alisema, ushindani kati ya Marekani na China ni mgongano kati ya staarabu tofauti. Kauli hiyo imewashangaza wamarekani na dunia nzima, na wengi wanaona kuwa, kauli hiyo inapaka matope ustaarabu, na kuifanya wizara ya mambo ya nje ya Marekani iwe kama mchekeshaji.

  Bibi Skinner alisema ushindani kati ya Marekani na China ni mgongano mkubwa kati ya staarabu. Kauli hiyo inatokana na mawazo ya mtaalamu wa mambo ya siasa wa Chuo Kikuu cha Harvard cha Marekani Bw. Samuel Huntington. Baada ya vita baridi, Bw. Huntington alitoa mawazo yake kuhusu mgongano kati ya staarabu, ambayo yalilaumiwa na watu wengi. Hata hivyo kufuatia mawazo hayo, Bw. Huntington alizionya nchi za magharibi zisijaribu kubadilisha ustaarabu usio wa kimagharibi, na kuhimiza mazungumzo, maelewano na ushirikiano kati ya staarabu tofauti. Bibi Skinner alielewa vibaya mawazo ya Bw. Huntington, na kutaka kuchochea mgongano kati ya staarabu.

  Aidha Bibi Skinner haelewi vizuri mambo ya siasa za Marekani na uhusiano kati ya Marekani na China. Alisema Marekani haijawahi kuwa na migogoro ya ustaarabu zamani kama ilivyo kati yake na China. Lakini ukweli ni kwamba baada ya shambulizi la kigaidi la Septemba 11, Marekani ilianzisha vita mbili katika eneo la Mashariki ya Kati, na kutoa sera ya kuwadharau waislamu. Lakini Marekani ilikataa kutaja kuwa huu ni mgongano kati ya staarabu, kwani inafahamu vizuri kuwa baadhi ya mambo yanaweza kufanywa kisiri tu.

  Jambo lingine linalowashangaza zaidi wasomi wa Marekani ni kwamba, Bibi Skinner alisema hii ni mara ya kwanza ya Marekani kuwa na nchi kubwa adui ambayo wananchi wake si wazungu, kwani mgongano wa zamani kati ya Marekani na Umoja wa Kisovieti ulikuwa ni mgongano kati ya wazungu. Huu ni ubaguzi halisi wa rangi, hivyo wasomi wengi wa Marekani wameeleza kutokubali kauli hiyo.

  Lakini kusema kweli, kauli ya Bibi Skinner ni maoni ya pamoja ya baadhi ya wamarekani. Marekani inajidai kuwa kinara halisi wa ustaarabu wa kizungu, lakini inafuata kanuni ya "wanyama wakubwa kula wanyama wadogo". Habari zinasema wizara ya mambo ya nje ya Marekani inatunga mkakati dhidi ya China kufuatia mawazo ya mgongano kati ya staarabu tofauti.

  Ustaarabu si wa kipekee, na ustaarabu wowote hauwezi kuenezwa dunia nzima. Ustaarabu wote ni mali ya binadamu. Katika maelfu ya miaka iliyopita, ustaarabu wa mashariki na ustaarabu wa sehemu nyingine umeheshimiana na kushirikiana vizuri. Duniani hakuna mgongano wa staarabu, mtu yeyote akitaka kuleta mgongano wa staarabu, atapingwa na watu wote wapenda amani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako