• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hatua ya Marekani kuongeza ushuru wa forodha haitatatua masuala kati yake na China

    (GMT+08:00) 2019-05-14 19:32:48

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo amesema, hatua ya Marekani kuongeza ushuru haitasaidia kutatua masuala kati yake na China, na kwa Marekani kuanzisha vita vya kibiashara hakutakuwa na manufaa kwa nchi hiyo na jamii ya kimataifa. Geng Shuang amesema, China haitaki na haipendi kupigana vita vya kibiashara, lakini kamwe haiogopi, na kwamba China haitashindwa nashinikizo lolote kutoka nje, na ina nia na uwezo wa kulinda maslahi yake halisi.

    Bw. Geng Shuang pia amesema, China siku zote inazingatia uaminifu na kutimiza ahadi yake, imeonyesha udhati na wema katika mazungumzo ya kiuchumi na biashara kati yake na Marekani, na inatumai Marekani inaweza kuendana na China.

    Habari zinasema, rais Donald Trump wa Marekani amesema kwenye Twitter yake kuwa, China imevunja baadhi ya ahadi zake wakati mazungumzo ya kiuchumi na kibiashara yamefikiwa kwa asilimia 95, na kulaumu China kusababisha kukwama kwa mazungumzo hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako