• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tahariri ya CMG yafafanua nia na nguvu ya China katika vita vya kibiashara na Marekani

  (GMT+08:00) 2019-05-14 20:22:09

  Tahariri iliyotolewa jana na televisheni ya Shirika kuu la Utangazaji la China CGM. Tahariri hiyo inayozungumzia vita vya kibiashara vilivyochochewa na Marekani na msimamo wa China imefuatiliwa sana na watazamaji wa China.

  Tahariri hiyo imesema China imeweka wazi msimamo wake mapema, ambao ni haivipendi, wala haiviogopi. Imesema bila kujali mabadiliko yalivyo duniani, kazi muhimu zaidi ya China ni kushughulikia vizuri mambo yake yenyewe, kuimarisha mageuzi na kufungua mlango zaidi, ili kutimiza maendeleo yenye sifa nzuri ya uchumi. Kama rais Xi Jinping wa China alivyosema, uchumi wa China ni bahari, si dimbwi, kwani kimbunga kinaweza kuangamiza dimbwi, lakini hakiwezi kuangamiza bahari.

  Kwa kukabiliwa na shinikizo kubwa la Marekani, China imesema haitarudi nyuma katika maslahi kuu, wakati huohuo, haitafunga mlango wa mazungumzo.

  China ilitangaza hatua yake ya kulipiza kisasi kwa Marekani baada ya nchi hiyo kuongeza ushuru wa forodha wa bidhaa zake. Habari hizi zilisababisha msukosuko katika soko la fedha duniani, haswa hisa ya Marekani imeshuka kwa kiasi kikubwa. Aidha, ripoti iliyotolewa na Shirika la Goldman Sachs inasema, ongezeko la ushuru wa bidhaa kutoka China limezidisha mzigo kwa wateja wa Marekani. Hali hii inaonesha kuwa vita vya kibiashara vinaleta hasara kwa China, Marekani na dunia nzima.

  Hadi sasa China na Marekani zimefanya duru 11 za mazungumzo kuhusu suala la biashara. China imetambua kuwa si rahisi kufikia makubaliano, na mgongano wa kibiashara kati nchi hizo mbili utaweza kuwa wa muda mrefu. Lakini, katika mchakato wa kutimiza ustawi tena wa taifa la China, mgongano huo ni tatizo dogo, China inajiamini kuwa inaweza kushinda changamoto zote hatimaye.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako