• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China ahutubia ufunguzi wa mazungumzo ya ustaarabu ya Asia

  (GMT+08:00) 2019-05-15 20:04:58

  Mazungumzo ya ustaarabu ya Asia leo yamefunguliwa hapa Beijing. Rais Xi Jinping wa China amehudhuria ufunguzi huo na kutoa hotuba ya "kuzidisha mawasiliano ya ustaarabu, na kujenga jumuiya ya Asia yenye hatma ya pamoja".

  Mazungumzo ya ustaarabu ya Asia yalipendekezwa na rais Xi Jinping wa China kwenye mkutano wa kilele wa uaminifu wa Asia uliofanyika mwaka 2014 na mkutano wa Bo'ao wa mwaka 2015. Kwenye hotuba yake Rais Xi ameelezea umuhimu wa binadamu kuwasiliana. Anasema,

  "Hivi sasa, hali ya kuwepo kwa ncha nyingi duniani, mafungamano ya uchumi, anuwai ya utamaduni, maendeleo ya jamii ya habari imeleta matumaini mazuri kwa binadamu wote. Wakati huohuo, kutokana na unyeti na utatanishi wa hali ya kimataifa, binadamu tunakabiliwa na changamoto mbalimbali, ambazo zinahitaji nchi zote duniani kushirikiana vizuri ili kukabiliana nazo. Mazungumzo ya ustaarabu ya Asia yatatoa jukwaa jipya kwa nchi za Asia na dunia nzima kufanya mazungumzo na mawasiliano ya ustaarabu."

  Rais Xi amependekeza kuongeza mawasiliano na maelewano kati ya nchi tofauti, makabila tofauti na ustaarabu tofauti, ili kuimarisha msingi wa watu na ustaarabu wa jumuiya ya binadamu yenye mustakbali wa pamoja. Amesisitiza kuwa binadamu wana tofauti ya rangi, lakini hakuna tofauti ya ngazi. Anasema,

  "Ustaarabu wote una mzizi maalumu, na unawakilisha busara na matumaini ya nchi au kabila. Watu wanaodhani kuwa wana rangi na ustaarabu bora zaidi kuliko wengine ni wajinga, na wataleta taabu kubwa. Tunapaswa kufuata usawa na kuheshimiana, kuacha kujigamba na ubaguzi, kuhimiza mazungumzo kati ya ustaarabu tofauti, na kuuwezesha kuishi pamoja kwa masikilizano."

  Ili kuhimiza mawasiliano ya ustaarabu kati ya China na nchi nyingine za Asia, rais Xi ametoa mapendekezo kadhaa, yakiwemo kuhifadhi mali za urithi za utamaduni wa Asia, kutafsiri vitabu maarufu vya Asia kwa lugha tofauti, kuongeza ushirikiano katika sekta ya tamthiliya na filamu, kuunda mtandao wa mawasiliano na ushirikiano kati ya washauri mabingwa, na kuhimiza utalii barani Asia. Rais Xi amewaeleza wajumbe wa mazungumzo hayo kuwa, China itafungua mlango zaidi kwa dunia. Anasema,

  "Kuzitendea vizuri nchi majirani na kusikilizana na nchi nyingine, ni desturi ya taifa la China kutoka zama za kale. Hivi leo China si nchi ya China tu, bali ni nchi ya Asia, na ni nchi ya dunia. Katika siku zijazo, China itaambatana na dunia kwa kufungua mlango zaidi, na kuchangia ustaarabu wake wenye uhai zaidi."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako