• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Marekani lasema liko kwenye hali ya tahadhari nchini Iraq na Syria kutokana na vitisho vya Iran

    (GMT+08:00) 2019-05-15 17:22:27

    Jeshi la Marekani limesema mapema leo kuwa vikosi vyake viko kwenye hali ya tahadhari nchini Iraq na Syria kutokana na hofu ya vitisho kutoka kwa makundi yanayoungwa mkono na Iran katika kanda hiyo.

    Msemaji wa Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani Bw. Bill Urban amesema, hali hiyo ya tahadhari imetokana na uwezekano wa taarifa za kiintelijensia za vitisho kutoka kwa wenza wa Marekani kuhusu makundi yanayoungwa mkono na Iran katika kanda hiyo.

    Marekani pia imeongeza askari wake katika eneo hilo hivi karibuni kwa kupeleka meli ya kubeba ndege, ndege za kudondosha mabomu, na mfumo wa kuzuia makombora, kwa madai ya tishio la kushambuliwa na Iran.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako