• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Faida ya Vodacom yapanda

    (GMT+08:00) 2019-05-15 17:22:27
    Licha ya misukosuko kadhaa inayokabiliana nayo, mapato ya Vodacom yamevuka Sh 1 trilioni kwa mwaka unaoishia Machi 31na faida yake kabla ya kodi kuongezeka kwa asilimia 29.7. Ndani ya kipindi hicho, taarifa za fedha za kampuni zinaonyesha ilipita Sh 1.02 trilioni ikilinganishwa na Sh 977.99 bilioni ilizopata mwaka ulioishia Machi 31, 2018.

    Kutokana na mapato hayao, faida ya utendaji au faida kabla ya kodi, ilifika Sh 115.33 bilioni kutoka Sh 88.9 bilioni iliyopta mwaka jana, lakini faida halisi ikashuka kutoka Sh 170.24 bilioni iliyopatikana mwaka jana hadi Sh 90.76 bilioni mwaka huu.

    Faida halisi kubwa ya mwaka jana, tarifa zinaonyesha ilichangiwa na mauzo ya mali ya kudumu na si shughuli za biashara za kampuni hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako