• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sekta ya setilaiti nchini China yaendelea kwa kasi

    (GMT+08:00) 2019-05-15 18:42:41

    Thamani ya jumla ya sekta ya huduma ya mfumo wa satelaiti wa safari na maelekezo nchini China imefikia dola za kimarekani bilioni 43.93 mwaka jana, ikiwa ni ongezeko la asilimia 18.3 kuliko mwaka 2017.

    Hayo yamo kwenye takwimu zilizotolewa katika Waraka Mweupe kuhusu Maendeleo ya Sekta ya Huduma ya Mfumo wa Safari na Maelekezo (2019). Sekta muhimu ambazo zinahusiana moja kwa moja na maendeleo na utumiaji wa teknolojia ya mfumo wa safari wa satelaiti ni pamoja na chip, vifaa vya kielektroniki, software na miundombinu, ambazo thamani yake ilifikia dola bilioni 15.58 za kimarekani.

    Mfumo wa Satelaiti za kuongoza mawasiliano wa Beidou (BDS) umechangia asilimia 80 katika thamani ya jumla iliyotokana na sekta hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako