• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Wakulima kutoka kaunti ya Vihiga kupewa mbegu za parachichi

    (GMT+08:00) 2019-05-15 19:14:01

    Gavana wa kaunti ya Vihiga nchini Kenya Wilbert Ottichilo, amenzisha mradi wa kusambaza mbegu za parachichi kwa wakulima 20,000 kutoka kaunti hiyo. Hii inafuatia mkataba uliotiwa saini kati ya Kenya na China. Kwenye mkataba huo wa mwezi jana, Kenya itakuwa ikiuza asalimia 40 ya parachichi zake kwa taifa la China. Shughuli hii ya kusambaza mbegu za parachichi itagharimu serikali ya kaunti ya Vihiga shilingi milioni 4.5. Itachukuwa muda wa miezi 16 kwa mbegu hizi kukomaa na kasha parachichi kusafirishwa hadi China. Wakulima 20,000 watakaonufaika na mradi huu hawatalipia chochote kupata mbegu za parachichi.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako