• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marekani yajidanganya kwa kusema inaibiwa

  (GMT+08:00) 2019-05-15 20:03:01

  Hivi karibuni baadhi ya wanasiasa wa Marekani wanadai kuwa nchi hiyo ni kama sanduku la kuhifadhi pesa, na nchi nyingine zote ikiwemo China zinaiba pesa kutoka kwake, jambo linalodhihirisha kuwa wanaosema hivyo hawana ufahamu mpana kuhusu masuala ya uchumi.

  Utaratibu wa soko unaonesha kuwa, biashara ikifanywa kwa hiari, ni lazima inanufaisha pande mbili, na ushirikiano wa biashara kati ya China na Marekani pia ni hivyo. Katika miaka mingi iliyopita, ushirikiano huo umehimiza maendeleo ya uchumi wa nchi hizo mbili na kuinuka kwa kiwango cha sekta za uchumi. Lakini Marekani haitilii maanani hali hiyo, na kutoa kauli zisizo na ukweli kuhusu China, kwa kusema China inaiba teknolojia, ajira na mitaji ya Marekani, na inafanya hivyo ili kupata kisingizio kwa ajili ya kitendo chake cha kuongeza ushuru wa forodha kwa bidhaa za China.

  Lakini ukweli daima hudhihirika. Takwimu zinaonesha kuwa, Marekani imepata faida kubwa kutoka China. Kwa mfano, mwaka 2017, China ililipa Marekani dola bilioni 7.13 kwa matumizi ya hakimiliki za kiubunifu. Hivi sasa mauzo ya bidhaa za kampuni za Marekani nchini China yanafikia dola bilioni 700 za kimarekani kwa mwaka, na kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2017, mauzo ya bidhaa za Marekani kwa China yameongezeka kwa asilimia 86, huku ongezeko hilo katika nchi nyingine ni asilimia 21 tu.

  Hivi sasa zaidi ya asilimia 70 ya biashara za kimataifa zinahesabiwa kwa dola za kimarekani, na hali hii inaleta fadia ya matrilioni ya dola kwa nchi hiyo. Mbali na hayo, Marekani inanyang'anya mali za nchi nyingine kwa kuchapisha fedha kwa wingi.

  Hata hivyo, sasa Marekani inalaumu nchi nyingine kuiba fedha zake. Kauli hiyo inatokana na udhaifu wa sekta zake za uzalishaji na ukosefu wa uwezo wa kukabiliana na hali hiyo.

  Bw. Lawrence Summers aliyekuwa waziri wa fedha wa Marekani amesema, uwezo wa juu wa China katika baadhi ya teknolojia unatokana na uwekezaji mkubwa na mfumo bora wa elimu, na badala ya kuzuia maendeleo ya China, Marekani inapaswa kuendeleza teknolojia zake zaidi ili kudumisha hadhi yake.

  Katika miaka 40 iliyopita tangu China ianze kutekeleza mageuzi na ufunguaji mlango, mafanikio makubwa yaliyopatikana hayakuibwa au kufadhiliwa na nchi nyingine, bali yanatokana na juhudi za wananchi wote wa China. Marekani haiwezi kudanganya dunia, wala kuzuia maendeleo ya China. China itafungua mlango zaidi, na kufanya vizuri mambo yake, ili kutengeneza miujiza mingine.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako