• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uchambuzi: ustaarabu wa binadamu hauna mzuri wala mbaya

  (GMT+08:00) 2019-05-15 20:40:17

  Mkutano wa mazungumzo ya ustaarabu ya Asia umefunguliwa leo hapa Beijing. Rais Xi Jinping wa China amehutubia ufunguzi wa mkutano huo na kufafanua wazo la China kuhusu mawasiliano na maingiliano ya ustaarabu wa wa Asia na wa binadamu wote. Amesisitiza kuwa, binadamu wana tofauti ya rangi za ngozi na lugha, ustaarabu hauna mzuri wala mbaya.

  Wazo hilo limepongezwa na viongozi wa nchi mbalimbali, maofisa, wasomi na wajumbe wa vyombo vya habari wanaohudhuria mkutano huo.

  Katika siku za karibuni, baadhi ya wanasiasa wa nchi za magharibi wanachochea kwa makusudi raundi mpya ya kauli za mgongano kati ya staarabu tofauti, na kusema, nchi zenye ustaarabu tofauti hakika zitakuwa na mgogoro. Chini ya hali hiyo, pande mbalimbali zimesifu kuwa mkutano huo wa mazungumzo ya ustaarabu ya Asia umefanyika kwa wakati.

  Binadamu wanapokabiliana na changamoto za pamoja wanahitaji nguvu za utamaduni na ustaarabu. Asia inataka kutimiza amani, utulivu, ustawi wa pamoja, kufungua mlango na kushirikiana, na ili kufanya hivyo, siyo tu inahitaji nguvu za uchumi na teknolojia, bali inahitaji nguvu za utamaduni na ustaarabu. Rais Xi amesisitiza kuwa, inahitaji kuheshimiana na kutendeana kwa usawa kati ya staarabu tofauti. Kila ustaarabu una thamani yake. Wale wanaoona spishi yao na ustaarabu wao ni wa juu kuliko wengine, na wanashikilia kubadilisha ustaarabu wa wengine hata kuchukua nafasi za wengine, sio wastaarabu.

  Ustaarabu unataka kuendelezwa daima, ni lazima kufanya mawasiliano na maingiliano, na watu ni njia nzuri ya kufanya mawasiliano ya ustaarabu. Katika mwaka 2018, wachina zaidi milioni 160 walitalii nchi za nje, pia China imepokea watalii kutoka nchi za nje karibu milioni 140. Wachina wengi zaidi wanajionea ustaarabu tofauti, vilevile, wageni wengi zaidi wanahisi uhai wa maendeleo ya uchumi wa China na utamaduni wa kichina ambao ni tofauti na vitabu vyao.

  Katika hotuba yake ya leo, rais Xi alitoa kauli hii, "tunapaswa kufanya ustaarabu wa nchi yetu uwe na uhai zaidi, pia tunapaswa kuweka mazingira kwa maendeleo ya ustaarabu wa nchi nyingine, ili ustaarabu wa nchi mbalimbali duniani kustawisha kwa pamoja". Kauli hiyo imepongezwa na watu wengi, kwa sababu wanaona kuwa, China katika mchakato wake wa kujenga mustakabali wake mzuri, itakuwa wazi zaidi na kuchangia dunia kwa ustaarabu wake wenye uhai zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako