• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Guardiola achaguliwa kocha bora wa msimu, awapita Klopp na Pochettino, sasa awekwa kundi moja na Ferguson na Mourinho

  (GMT+08:00) 2019-05-16 09:35:53

  Kocha mkuu wa mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza Manchester City Pep Guardiola, ameshinda tuzo ya kocha bora wa msimu wa 2018/19 wa ligi hiyo.

  Guardiola amefanikiwa kushinda tuzo hiyo mara ya pili mfululizo baada ya kuisaidia klabu yake ya Man City kubeba ubingwa huo na kuwashinda Jurgen Klopp, Mauricio Pochettino na Nuno Espirito Santo ambao waliingia fainali kwenye kinyang'anyiro hicho.

  Mbali na kutwaa tuzo hiyo ya kocha bora, Pep Guardiola ameingia kwenye rekodi ya kuwa miongoni mwa mameneja watatu waliyofanikiwa kutwaa ubingwa huo wa ligi kuu mara mbili mfululizo baada ya kufanya hivyo Sir Alex Ferguson na Mreno Jose Mourinho.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako