• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • GOFU: Tiger Woods apiga tizi la nguvu kujiandaa kwa ubingwa wa PGA

    (GMT+08:00) 2019-05-16 09:36:33

    Bingwa wa mchezo wa gofu Tiger Woods ameanza mazoezi ya raundi ya pili kujiandaa na michuano ya 101 ya ubingwa wa PGA, ambayo ni ya pili mikubwa kwa mwaka. Michuano hiyo itafanyika Berthpage Black jijini New York Marekani.

    Woods ambaye alikaa miaka 11 bila ya kushinda taji lolote, aliondoa gundu hilo kwa kutwaa taji la michuano ya Masters mwezi uliopita na sasa anawania taji la 16 kubwa tangu aanze kushiriki mashindano ya gofu. Wiki iliyopita Tiger Woods alitunukiwa medali ya rais ya uhuru na rais wa Marekani Donald Trump katika hafla iliyofanyika Ikulu nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako