• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • NDONDI: Mwakinyo azidi kutesa kwa viwango vya ubora duniani

  (GMT+08:00) 2019-05-16 09:37:51

  Hassan Mwakinyo bondia wa Tanzania uzito wa kati, amepanda nafasi nne za mabondia bora duniani kwenye orodha ya viwango iliyotolewa na mtandao maarufu wa ngumi za kulipwa Boxrec.

  Mwakinyo ambaye alikuwa nafasi ya 22 kati ya mabondia 1,515 amepanda hadi nafasi ya 18 katika orodha hiyo iliyotolewa jana. Bondia huyo pia anashika namba moja barani Afrika na katika viwango vya Tanzania.

  Akizungumzia mafanikio hayo, Mwakinyo amesema, juhudi ya mazoezi na kufuata maagizo ya mwalimu ndio zimemfikisha hapo na ushindi wa TKO katika raundi ya tano dhidi ya bondia wa Argentina, Sergio Gonzalez umempandisha chati.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako