• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Gor Mahia yanusa ubingwa Kenya, yabakiza alama 6 tu

  (GMT+08:00) 2019-05-16 09:38:11

  Mabingwa wa ligi kuu ya soka ya Kenya, Gor Mahia wamebakisha alama sita tu kabla ya kutetea tena taji la ubingwa wa ligi hiyo msimu huu baada ya juzi kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Sofapaka katika mchezo uliochezwa uwanja wa Moi mjini Kisumu.

  Samuel Onyango na Jacques Tuyisenge walifunga magoli hayo katika kipindi cha pili na kuifanya Gor Mahia kufikisha alama 66. Sofapaka wamebaki na alama zao 56 wakisalia katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi hiyo.

  Kocha wa Gor Mahia Hassan Oktay amesema sasa ana uhakika wa kutetea ubingwa kwasababu wameongeza tofauti ya alama kati yao na anayewafuatia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako