• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Zambia yasifu mipango ya kufundisha lugha ya kichina shuleni

  (GMT+08:00) 2019-05-16 09:40:35

  Katibu wa kudumu kwenye Wizara ya Elimu ya Juu ya Zambia Bw. Mabvuto Sakala ameipongeza serikali ya Zambia kwa uamuzi wa kufundisha lugha ya kichina katika shule nchini humo, akisema hatua hii itasaidia kupunguza vikwazo vya mawasiliano na wachina wanaofanya kazi nchini humo.

  Bw. Sakala amesema kiwango cha lugha ya kichina kitapimwa na mamlaka ya elimu ya nchi hiyo kuanzia mwaka ujao. Pia amesema makubaliano kuhusu mafunzo ya lugha ya kichina yatakayofikiwa kati ya Taasisi ya Confucius ya China na waziri wa elimu wa Zambia, yatazindua rasmi utekelezaji wa mafunzo ya lugha ya kichina kwenye shule za sekondari nchini humo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako