• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Gharama ya maisha kupanda zaidi kwa ajili ya mafuta

  (GMT+08:00) 2019-05-16 19:18:02
  Wakenya wanatarajiwa kukumbana na hali ngumu ya maisha kwa kipindi cha mwezi mmoja ujao, baada ya Tume ya Kudhibiti Kawi (ERC) kutangaza bei mpya ya mafuta inayoongezeka kwa zaidi ya shilingi tano.

  Kwenye taarifa ya kubadilisha bei za mafuta ya petrol, mafuta ya dizeli na ya taa ERC ilieleza kuwa imesukumwa kuchukua hatua hiyo kwa sababu ya kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo muhimu katika soko la kimataifa.

  Inakadiriwa kuwa ongezeko hilo huenda likaathiri bei za bidhaa muhimu zinazotegemea mafuta, mbali na kushuhudiwa kupanda kwa nauli. Katika mabadiliko hayo, mafuta ya petroli yalipanda kwa Sh5, dizeli kwa Sh2 na mafuta taa kwa zaidi ya Sh2. Japokuwa bei ya mafuta ilipungua mwishoni mwa Februari na kufikia hata Sh99 kwa lita jijini Nairobi, inaonekana serikali imeanza upya kuongeza kidogo kidogo ushuru huo ili kurejesha ulipodhamiriwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako