• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wafanyabiashara wa China waonyeshwa fursa

  (GMT+08:00) 2019-05-16 19:18:30
  Wafanyibiashara wa China wametakiwa kuwekeza katika usindikaji wa mazao ya chakula kwa kutumia malighafi inayopatikana nchini Tanzania ili kutosheleza mahitaji ya soko ifikapo mwaka 2050 ambapo inakadiriwa asilimia 50 ya watu barani Afrika watakuwa wamekimbilia maeneo ya mijini.

  Wito huo ulitolewa na Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) nchini humo Bi Angela Kairuki, wakati akifungua kongamano la uwekezaji kati ya China na Tanzania katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).

  Kairuki alisema kuwa mahitaji ya chakula yatakuwa makubwa kutokana na ongezeko kubwa la watu wanaokimbia uchumi wa vijijini wa kilimo na kwenda mijini kutafuta kazi za viwandani na huduma.

  Alisema Tanzania ina ardhi nzuri yenye rutuba pamoja na maji ya kutosha, hivyo kuwezesha uzalishaji wa mazao yanayotumiwa sana na jamii barani Afrika kama vile nafaka, maharage, mihogo, viazi vitamu na matunda ya aina mbalimbali yakiwamo maparachichi.

  Aidha, Kairuki alisema fursa nyingine ni usindikaji wa nyama pamoja na samaki ambapo alibainisha kuwa kuna mahitaji makubwa sana kwa soko la nchi za Asia.

  Kairuki ameongeza kuwa mpaka sasa Tanzania ina soko la uhakika kutokana na kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) yenye watu milioni 152 na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) yenye watu milioni 800.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako