Mji wa Nakuru ni wa nne kwa ukubwa nchini Kenya baada ya Nairobi, Kisumu na Mombasa. Pia ni makao makuu ya jamii za bonde la ufa.
Uwekezaji katika sekta ya viwanda aidha umepungua, kufuatia madeni yanayotokana na mikopo ya benki, huku wafanyakazi waliopigwa kalamu bila mshahara wakielekea kortini kusaka haki ya malipo yao.
Viwanda vingi vimegeuzwa kuwa sehemu za kufanyia biashara ndogo ndogo, huku majengo ya mashirika ya kibinafsi yakiuzwa.
Hivi sasa viwanda vingi vimegeuzwa sehemu za kuhifadhi bidhaa kwa bei nafuu.
Muungano wa Watengenezaji wa Bidhaa (KAM) uliweka matawi yake mengi kaunti ya Nakuru 1966, miaka michache tu baada ya Kenya kupata uhuru lakini sasa taswira ni tofauti. Baadhi ya viwanda katika kaunti ya Nakuru bado vinaendelea kudumu huku vingine vikininginia ama kubakia tupu shughuli zikionekana kusimama.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |