• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi linaloongozwa na Saudi Arabia lafanya shambulizi la anga kwenye mji unaoshikiliwa na waasi, Yemen

    (GMT+08:00) 2019-05-16 19:42:46

    Jeshi linaloongozwa na Saudi Arabia limefanya mashambulizi ya anga kwenye maeneo yanayokaliwa na waasi katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa mapema leo, na kusababisha vifo vya watu sita na uharibifu wa mali.

    Wizara ya afya inayoongozwa na waasi imesea, katika shambulizi hilo, zaidi ya watu 30 pia wamejeruhiwa, na huenda idadi ya vifo ikaongezeka kwa sababu baadhi ya majeruhi wako kwenye hali mbaya.

    Kituo cha televisheni cha Houthi cha al-Masirah pia kimeripoti kuwa, nyumba moja iliyo karibu na shule pia ilishambuliwa, na kusababisha idadi isiyojulikana ya vifo na majeruhi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako