• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RAGA: Refa mzoefu kusimamia fainali Kabras na KCB

    (GMT+08:00) 2019-05-17 09:54:24

    Refa mwenye uzoefu mkubwa katika ulingo wa raga, Moses Ndung'u ameteuliwa na shirikisho la raga nchini Kenya (KRU) kusimamia fainali ya ubingwa wa raga itakayowakutanisha Kabras Sugar na KCB wikendi hii mjini Kakamega.

    Ndung'u aliyemiminiwa sifa kuwa mwamuzi wa fainali ya kipute cha Impala Floodlit mwaka 2018, atasaidiwa na Constant Cap na Godwin Karuga.

    Wanabenki wa KCB watachuana na Kabras Sugar kwenye fainali inayotarajiwa kuwa ya kusisimua zaidi na fungakazi ya msimu huu wa 2018-19. Katika safari yao ya kufuzu kwa fainali, KCB waliwabamiza Kenya Harlequins 46-13 katika uwanja wa Lion's Den, Nairobi huku wanasukari wa Kabras wakiyazima makali ya Mwamba RFC kwa alama 23-11

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako