• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yapoteza uaminifu kufuatia vitendo vyake

    (GMT+08:00) 2019-05-17 17:12:57

    Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa inasema, ikiwa nchi ya pili inayolipa ada zaidi kwa Umoja wa Mataifa, China imelipa ada zote za asilimia 12.01 ya bajeti ya umoja huo. Msemaji wa katibu mkuu wa umoja huo Bw. Stefan Dujarric ameishukuru China kwenye Twitter akitumia neno la kichina "Xiexie", lenye maana ya asante. Kwa upande wa Marekani, hadi tarehe mosi Januari mwaka huu, imechelewa kulipa ada ya kawaida ya Umoja wa Mataifa ambayo ni dola za kimarekani milioni 381, na ada ya kijeshi dola milioni 776.

    Hivi sasa ukubwa wa uchumi wa Marekani umezidi dola trilioni 20 za kimarekani, na Marekani ingebeba mizigo ya asilimia 22 ya bajeti ya kawaida na asilimia 28 ya bajeti ya kijeshi ya Umoja wa Mataifa. Lakini jambo la kuwashangaza watu ni kwamba, Marekani kwa mara nyingi imedai kupunguza mizigo hiyo, na kuchelewa kulipa ada zilizoamuliwa na umoja huo.

    Tangu serikali mpya ya Marekani iingie madarakani, nchi hiyo imejitoa kwenye Makubaliano ya Paris juu ya suala la mabadiliko ya hali ya hewa, Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, Kamati ya Haki za Binadamu ya umoja huo, na Makubaliano kuhusu Suala la Nyukilia la Iran. Mbali na hayo, inafikiria kujitoa kwenye Makubaliano ya Biashara ya Silaha ya Umoja wa Mataifa. Wakati huohuo, Marekani imeinua fimbo ya ushuru wa forodha, na kujaribu kuzilazimisha China, Umoja wa Ulaya, Japan, Mexico, Canada na nchi nyinginezo zipokee makubaliano yasiyo na haki ya biashara. Kwani inaona kuwa utaratibu wa biashara ulioanzishwa na Marekani yenyewe sasa haulingani vizuri na maslahi yake, na inataka kuupindua na kujenga upya.

    Hali hii imewatanabahisha watu kuwa madhumuni ya Marekani kutetea "Marekani kwanza" ni kutaka kuweka maslahi yake juu ya utaratibu na kanuni za kimataifa.

    Hata hivyo, hii ni karne ya 21, na dunia haiwezi kurudi kwenye zama ya "samaki wakubwa kuwala samaki wadogo". Marekani inapoteza uaminifu wake kwa dunia kutokana na vitendo vyake vya kulinda maslahi yake.

    Hivi sasa licha ya China kupinga Marekani kuongeza ushuru wa forodha kwa bidhaa zake, Umoja wa Ulaya pia umesema, ili kukabiliana na Marekani kujaribu kuongeza ushuru wa forodha kwa magari ya umoja huo, nao unaorodhesha bidhaa za Marekani ili kulipiza kisasi. Kwenye mazungumzo ya biashara kati ya Marekani na Japan yaliyofanyika Aprili, Japan ilikataa sharti la Marekani la kupunguza au kuondoa ushuru wa forodha kwa bidhaa za mazao ya Marekani.

    Methali ya kichina inasema, waaminifu hupata uungaji mkono, na wale wasio na uaminifu wataachwa na marafiki wote. Kwenye dunia yenye utandawazi na nchi nyingi, Marekani inajaribu kufunga mlango wake kutokana na sera yake ya "Marekani kwanza".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako