• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wang Yi akutana na mabalozi wa Umoja wa Ulaya na nchi wanachama wa umoja huo nchini China

    (GMT+08:00) 2019-05-17 20:27:27

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi leo hapa Beijing amekutana na mabalozi wa Umoja wa Ulaya na wa nchi 27 wanachama wa umoja huo nchini China.

    Bw. Wang amesema maslahi ya pamoja kati ya China na Umoja wa Ulaya ni makubwa kuliko tofauti. Pande mbili zinapaswa kuimarisha mawasiliano, kulinda kanuni ya kimsingi ya uhusiano wa kimataifa na mfumo wa biashara wa pande nyingi, na kushirikiana kuhimiza maendeleo ya ustaarabu wa binadamu na maendeleo ya jamii.

    Mabalozi hao wanasema Umoja wa Ulaya na China zinashikilia hali ya pande nyingi, kuhimiza biashara huria kunaendana na maslahi ya pande mbili, pia ni muhimu kwa utulivu na maendeleo ya dunia. Pia wamesema Umoja wa Ulaya unapenda kushiriki kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako