• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Huawei yachukua hatua kali kujibu vikwazo ilivyowekewa na Marekani

  (GMT+08:00) 2019-05-19 19:07:55

  Wizara ya biashara ya Marekani imetangaza kuiweka kampuni ya Huawei ya China na mashirika yake mengine 70 katika orodha yake nyeusi, ili kuizuia Huawei kununua teknolojia au vifaa kutoka kampuni za Marekani. Kitendo hicho kinalenga kuzuia maendeleo ya teknolojia ya juu ya China na kulinda hadhi ya Marekani kuwa kinara duniani katika sayansi na teknolojia. Lakini kampuni ya Huawei imeanzisha haraka mpango mbadala uliotafitiwa kwa miaka zaidi ya kumi, na kuhakikisha usalama wa kimkakati wa bidhaa nyingi za Huawei na uzalishaji mfululizo wa bidhaa zake. … ana maelezo zaidi.

  Kupitia maendeleo ya kimataifa ya miaka zaidi ya 20, kampuni ya Huawei ikiwa mtengenezaji mkubwa zaidi wa vifaa vya mtandao duniani imeanzisha shughuli zake katika nchi zaidi ya 170 na kutoa huduma za Tehema kwa theluthi moja ya watu wote kote duniani. Lakini maendeleo ya kampuni hiyo nchini Marekani yamekwama. Kutoka kuzuiwa kwa manunuzi ya makampuni kadhaa ya Marekani hadi kufanyiwa uchunguzi unaodai kuwa kampuni hiyo inaharibu usalama wa taifa wa Marekani, Huawei siku zote imezuiwa nje ya soko la Marekani.

  Lakini Marekani bado ina wasiwasi mkubwa kutokana na Huawei kuongoza katika idadi ya hakimiliki ya ujuzi ya teknolojia ya 5G duniani. Mtandao wa 5G utakuwa medani mpya ya ushindani, Marekani ikiwa nchi inayoongoza katika sayansi na teknolojia duniani imedai kuwa mtandao wa 5G utakuwa mashindano ambayo lazima ishinde, pia hairuhusu uwepo wa mshindani yeyote mwengine. Kwa upande mmoja, Marekani inadai kuwa itashinda mashindano hayo kupitia ushindani badala ya vikwazo, kwa upande mwingine, nchi hiyo inatumia nyenzo za sera ya kujilinda kibiashara kuzuia maendeleo ya kampuni ya Huawei kwa kisingizio cha usalama wa taifa.

  Kitendo hicho hakijalinda usalama wa Marekani, bali kinyume chake kimeharibu faida ya makampuni ya Marekani yanayoshirikiana na Huawei, na kuathiri maelfu ya nafasi za ajira na kuharibu vibaya ushirikiano wa mnyororo wa utoaji wa bidhaa duniani.

  Kwa bahati nzuri, Huawei ikikabiliana na vikwazo hivyo vya Marekani, ilianza kufanya maandalizi katika miaka zaidi ya kumi iliyopita. Uzinduzi wa mpango mbadala umeonesha mkakati wake wa kuangalia mbali na wazo la kujiandalia kwa hali ya hatari. Moyo huo wa makampuni na wajasiriamali wa China umekuwa nguvu ya kuhimiza China kuendelea kupiga hatua kuelekea sayansi na teknolojia za hali ya juu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako