• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Serikali yaanza kushinikizwa kupunguza bei ya unga hadi dola 0.90

    (GMT+08:00) 2019-05-20 18:57:12

    Shirika la kutetea watumizi wa bidhaa limetishia kwenda mahakamani kuweka mikakati ya kupunguza bei ya unga wa mahindi hadi shilingi tisini. Shirika hilo, Consumer Downtown Association (CDA), linaitaka serikali kurejesha mpango wa unga wa bei nafuu ili kunusuru Wakenya dhidi ya makali ya njaa.

    Kulingana na shirika hilo, bei ya juu ya unga na bidhaa nyinginezo muhimu, imesababisha familia nyingi kupata mlo mmoja kwa siku au kulala tumbo tupu. Kwa sasa, kilo mbili za unga zinazuzwa kwa kati ya Sh120 na Sh150 katika maeneo mbalimbali nchini.

    Mnamo 2017, serikali ilitoa Sh6 bilioni kufadhili mradi wa kuagiza mahindi kutoka ughaibuni.

    Mpango huo ulisababisha kupungua kwa bei ya kugunia moja la kilo 90 kutoka Sh4,000 hadi Sh2,300. Kupitia mpango huo, bei ya unga wa mahindi ilipungua kutoka Sh153 hadi Sh90 kwa kila kilo 2 za mahindi.

    Ripoti ya Shirika la Takwimu nchini (KNBS) ilionyesha kuwa mfumko wa bei ya bidhaa ulivunja rekodi kwa kuongezeka kutoka asilimia 4.35 mnamo Machi hadi asilimia 6.58 mwezi Aprili.

    Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa mfumko wa bei ya bidhaa kufikia asilimia 6.58 katika kipindi cha miezi 19 iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako