• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya mambo ya nje ya China yasema Marekani inajaribu kutimiza matakwa yasiyo na msingi kupitia shinikizo la mwisho

    (GMT+08:00) 2019-05-20 19:53:31

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang amesema, sababu ya msingi ya kushindwa kwa duru ya 11 ya mazungumzo ya uchumi na biashara kati ya China na Marekani, ni Marekani inajaribu kutimiza matakwa yasiyo na msingi kupitia kuweka shinikizo la mwisho.

    Rais Donald Trump wa Marekani hivi karibuni amesema, Marekani na China zimefikia makubaliano fulani, lakini China imevuruga makubaliano hayo.

    Bw. Lu amesisitiza kuwa hajui makubaliano yaliyotajwa na Marekani, lakini Marekani siku zote huenda ina makubaliano inayoyatarajia ambayo hayajakubaliwa na upande wa China. Bw. Lu amesema udhati na msimamo wa kiujenzi uliooneshwa na China katika duru 11 zilizopita za mazungumzo umeshuhudiwa na jumuiya ya kimataifa. Amesisitiza tena kuwa mazungumzo ya uchumi na biashara kati ya China na Marekani yanaweza kupata mafanikio, kama yakifuata njia sahihi ya kuheshimiana na kunufaishana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako