• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasema wawekezaji wa kigeni wanapendelea China

  (GMT+08:00) 2019-05-21 19:54:42

  Rais Donald Trump wa Marekani amesema kuongeza ushuru kwa bidhaa za China kutazifanya kampuni zihamishe viwanda kutoka China kwenda Vietnam na nchi nyingine za Asia. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang amesisitiza kuwa wawekezaji wa kigeni wanapendelea China.

  Bw. Lu Kang amesema hayo kwenye mkutano wa waandishi wa habari, na kuongeza kuwa kitendo cha Marekani cha kuharibu kanuni za biashara kinaweza kuvuruga soko la kimataifa likiwemo la China na Marekani, na makampuni yanaweza kufanya chaguo kwa mwelekeo wa uwekezaji kwa mujibu wa mkakati wa mustakbali wa uchumi.

  Aidha Bw. Lu amesisitiza kuwa China siku zote inakaribisha makampuni ya kigeni kuwekeza nchini China na kufanya ushirikiano wa kunufaishana, na China itaendelea kutoa mazingira ya utulivu, haki, wazi na linaloweza kutarajiwa na uwekezaji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako