• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Ligi kuu Tanzania Bara- Simba Sports Club watetea ubingwa, shangwe kama lote.

  (GMT+08:00) 2019-05-22 08:18:27

  Ushindi wa mabao 2-0 walioupata Simba ya Dar es Salaam jana mbele ya Singida United kwenye uwanja wa Namfua umetosha kuwafanya wekundu hao wa Msimbazi kutetea kwa mara ya pili mfululizo ubingwa wao walioutwaa msimu uliopita.

  Mabao mawili yaliyopachikwa na Meddie Kagere dakika ya 9 na John Bocco dakika ya 60 yametosha kuwapa ubingwa na kuamsha shangwe kwa mashabiki wao kila kona.

  Simba imecheza jumla ya michezo 36 na imefikisha pointi 91 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kwenye ligi msimu huu, ikiwa bado na michezo miwili kibindoni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako