• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UN atoa mwito wa kuondoa vyanzo vilivyosababibisha watu kukimbia makwao barani Afrika

    (GMT+08:00) 2019-05-22 08:53:21

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana ametoa mwito wa kufanya juhudi ili kuondoa vyanzo vilivyosababisha watu kukimbia makwao barani Afrika.

    Akizungumza katika mkutano wa mazungumzo ya Afrika uliofanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York, Bw. Guterres amesema, njia bora zaidi ya kuwalinda wakimbizi ni kuwazuia wasiondoke kwenye makazi yao, ikimaanisha kushugulikia vyanzo vya kimsingi, ambavyo ni pamoja na umaskini, migogoro, ubaguzi na kutengwa kwa aina zote.

    Vilevile Bw. Guterres ametoa mwito wa kufuata Agenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa na Agenda ya 2063 ya Umoja wa Afrika, na kusisitiza kuwa kuondokana na umasikini ni kipaumbele cha taasisi hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako