• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mvutano wa biashara na sera za kimataifa zisizokuwa na uhakika vinaendelea kuathiri ongezeko la uchumi wa dunia

    (GMT+08:00) 2019-05-22 09:34:55

    Ripoti iliyotolewa na Shirika la Ustawi na Hali ya Uchumi wa Dunia la Umoja wa Mataifa WESP imesema, ongezeko la uchumi wa dunia limepungua kutokana na mvutano wa kibiashara, sera tete za kimataifa na upungufu wa imani ya biashara.

    Ripoti hiyo imesema, ongezeko la uchumi wa makundi ya kiuchumi yaliyoendelea na nchi nyingi zinazoendelea, limepungua kutokana na matatizo ya kimataifa na ya ndani.

    Habari zinasema, ongezeko la pato la dunia la mwaka huu lilipangwa kufikia asilimia 2.7, ambapo mwaka jana, makadirio yalikuwa ni asilimia 3.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako