• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa wito wa kushikilia kutatua suala la Libya kwa njia ya kisiasa

    (GMT+08:00) 2019-05-22 18:45:46

    Balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Ma Zhaoxu ametoa wito wa kushikilia kutatua suala la Libya kwa njia ya kisiasa.

    Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Libya, balozi Ma amesema China inazingatia sana maendeleo ya hali ya Libya. Amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kufuatilia zaidi suala la Libya, na kufanya juhudi kwa pamoja ili kuhimiza suala hilo litatuliwe haraka iwezekanavyo.

    Amesema China inashikilia siku zote kutatua suala ya Libya kwa njia ya kisiasa, na inataka pande zote husika zisimamishe mapambano haraka iwezekanavyo na kupunguza hali ya wasiwasi. Pia amesema jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuheshimu mamlaka, uhuru na ukamilifu wa ardhi wa Libya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako