• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mzinduzi wa Kampuni ya Huawei asema suala la msingi la biashara kati ya China na Marekani ni kiwango cha elimu

    (GMT+08:00) 2019-05-22 18:51:51

    Mzinduzi wa Kampuni ya Huawei ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji mkuu wa kampuni hiyo Bw. Ren Zhengfei amesema, elimu ya msingi na ya ufundi vinatakiwa kufuatiliwa zaidi, na suala la msingi la biashara kati ya China na Marekani ni kiwango cha elimu.

    Bw. Ren alipohojiwa na kituo kikuu cha redio na televisheni cha China CMG amesema, msingi wa nguvu ya nchi ni pamoja na miundombinu ikiwemo reli, barabara kuu, zana za mawasiliano barabarani, ujenzi wa miji, maji ya bomba, lakini miundombinu haina roho, roho ya nchi iko katika utamaduni, falsafa, elimu na kiwango cha utamaduni cha binadamu.

    Amesema amechunguza elimu za kote duniani na kupata ufahamu na uelewa wa kina. Watoto ni siku za baadaye za taifa. Kama mkazo ukiwekwa kwenye kuwaelimisha watoto, baada ya miaka 20 hadi 30 wengi wao watakuwa watu wenye shahada za uzamili na uzamivu, ambao wataweza kutoa mchango katika sekta mpya za uvumbuzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako