• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tume ya uchaguzi ya Malawi yatoa mwito wa kuwepo kwa utulivu

    (GMT+08:00) 2019-05-22 19:31:58

    Tume ya uchaguzi ya Malawi imetoa mwito wa kuwepo kwa utulivu na uvumilivu miongoni mwa wananchi, wakati matokeo ya upigaji kura wa jana yanaendelea kusubiriwa.

    Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji Jane Ansah, amesema matokeo kutoka kwenye majimbo yameanza kufikia kwenye kituo kikuu cha kuhesabia kura, lakini yanatakiwa kuthibitishwa kabla ya kutangazwa. Amesema hakuna njia ya mkato zaidi ya kuhesabu kura, amewataka wamalawi waonyeshe uvumilivu wakati kura zinahesabiwa.

    Pia amewatahadharisha wananchi kuwa makini na mitandao ya jamii, ambayo inatoa matokeo ya uchaguzi, na kusema licha ya kuwa baadhi inasema ukweli, mingine inasema uongo na inaweza kusababisha vurugu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako