• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ndege za Rwanda kuanza safari ya China

    (GMT+08:00) 2019-05-22 20:58:22

    Shirika la Ndege la RwandaAir, linatarajia kuanza safari zake za kwenda Guangzhou, jiji ambalo ni la tatu kwa ukubwa nchini China. RwandaAir itasafiri Guangzhou mara tatu kwa wiki. Hii ni Jumanne, Alhamisi na Jumamosi. Ndege itakayotumiwa ni Airbus A330, ambayo ndiyo ndege ya kitaifa. Kuanzishwa kwa safari hizi kumechochewa na idadi kubwa ya wachina wanaokuja nchini Rwanda na raia wa Rwanda wanaokwenda China kwa sababu za kibiashara. Guangzhou utakuwa mji wa 28 kwa ndege za RwandaAir kutua, hii ni baada ya kuanza safari zake hadi Kinshasha, DR Congo.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako