• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Nigeria kuvunja baraza la mawaziri wiki ijayo

    (GMT+08:00) 2019-05-23 08:26:42

    Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria ameeleza nia yake ya kuvunja Baraza lake la Mawaziri jumanne ijayo, kabla ya kuapishwa kwa serikali mpya.

    Akizungumza katika mkutano wa baraza la mawaziri uliofanyika jana, ambapo huyo alikiri kuwa wa mwisho katika muhula wake wa kwanza wa urais, rais Buhari aliwaelekeza mawaziri wake kuendelea kutekeleza majukumu yao mpaka jumanne wiki ijayo. Pia amewaelekeza kukabidhi kazi zao kwa makatibu wakuu wa wizara zao, na pia kukabidhi barua za makabidhiano kwa Katibu wa Serikali ya Jamhuri katika siku hiyo.

    Waziri wa habari wa nchi hiyo Lai Mohammed amesema, serikali mpya itaapishwa Mei 29 katika Uwanja wa Eagle mjini Abuja.

    Rais Buhari alishinda uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi Februari mwaka huu, na hivyo anatarajiwa kuanza muhula wake wa pili madarakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako