• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika zatakiwa kutafuta suluhisho la kudumu la mgogoro wa wahamiaji

    (GMT+08:00) 2019-05-23 08:27:03

    Nchi na taasisi za Afrika zimetakiwa kutafuta suluhisho la kudumu la watu kulazimishwa kukimbia makazi yao barani humo, ikiwa ni siku chache kabla ya Siku ya Afrika itakayoadhimishwa jumamosi wiki hii.

    Kamati ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (ECA) imetoa wito huo na kusisitiza kuwa Afrika ina idadi kubwa ya watu waliolazimika kukimbia makazi yao duniani. Takwimu zilizotolewa na Kamati hiyo zinaonyesha kuwa, zaidi ya robo tatu ya watu milioni 68 waliolazimika kukimbia makazi yao wako Afrika. Chanzo cha mgogoro huo ni pamoja na mapigano, ukiukaji wa haki za binadamu, majanga ya kimaumbile, matatizo makubwa katika sekta ya afya na mgogoro wa kibinadamu.

    Siku ya Afrika ambayo huadhimishwa Mei 25 ya kila mwaka, inaashiria kuanzishwa kwa Umoja wa Muungano wa Afrika (OAU), kabla ya kuwa Umoja wa Afrika (AU), kwa lengo la kuboresha umoja na ustawi wa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako