• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Russia wakutana Bishkek

    (GMT+08:00) 2019-05-23 08:59:23

    Mjumbe wa taifa wa China na waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amekutana na mwenzake wa Russia Bw. Sergey Lavrov wakati alipohudhuria mkutano wa baraza la mawaziri wa mambo ya nje la nchi wanachama wa Shirika la Ushirikiano la Shanghai huko Bishkek.

    Bw. Wang Yi amesema, hivi sasa hali ya dunia inabadilika kwa haraka, China na Russia zinapaswa kufanya mawasiliano, kuimarisha ushirikiano wa kimkakati wa pande zote, na kulinda kanuni ya msingi ya mahusiano ya kimataifa na maslahi ya pamoja ya nchi hizo mbili. Amesema pande hizo mbili zinapaswa kufanya juhudi kwa pamoja na kufanya maandalizi mazuri kwa ajili ya ziara ya rais Xi Jinping wa China nchini Russia mwezi ujao na kuhudhuria Baraza la uchumi la kimataifa la Saint Petersburg.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako