• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani inajiumiza kwa kutumia "fimbo ya ushuru"

    (GMT+08:00) 2019-05-23 09:58:30

    Hivi karibuni baadhi ya watu wa Marekani wamesema, nchi hiyo imepata hasara kubwa kutokana na urari mbaya katika biashara na China, ambapo mamilioni ya ajira zimepotea. Wataalamu wa China wanaona kuwa, ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili unanufaisha pande zote, kauli ya Marekani haina msingi wowote, na Marekani itajiumiza kwa kutumia ovyo "fimbo ya ushuru".

    Katika miaka 40 iliyopita, biashara kati ya China na Marekani imeongezeka zaidi ya mara 230. Mkuu wa heshima wa Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo ya Taifa ya Chuo Kikuu cha Beijing Bw. Lin Yifu amesema, Marekani kununua bidhaa za China si kuifadhili China, biashara zinanufaisha pande zote mbili. Amesema,

    "Marekani inanunua bidhaa kutoka China, kwa kuwa Marekani haizalishi bidhaa hizo, na bidhaa za China zina bei nafuu na ubora mzuri. Hii ni kauni ya kimsingi ya biashara, na mtu yeyote mwenye elimu ya kawaida anafahamu hivyo."

    Ukweli ni kwamba, Marekani imenufaika sana kutokana na biashara na China. Takwimu zilizotolewa na Kamati kuu ya Biashara kati ya Marekani na China zinaonesha kuwa, biashara hiyo inaisaidia kila familia ya Marekani kupunguza matumizi ya dola 850 za kimarekani kwa mwaka. Mtafiti mwandamizi wa Kituo cha Utafiti wa Uhusiano kati ya China na Marekani cha Chuo Kikuu cha Qinghua Bw. Zhou Shijian anaona kuwa, China na Marekani zina viwango tofauti vya maendeleo, na pia zinachukua nafasi tofauti katika mnyororo wa thamani duniani. Marekani inapata faida kubwa kwa kudhibiti teknolojia za juu, ambapo China inapata faida ndogo kwa kuzalisha bidhaa za gharama nafuu.

    Aidha, wataalamu wanaona kuwa, chanzo cha urari mbaya katika biashara ya Marekani si China, bali ni matumizi makubwa kupita kiasi, upungufu wa akiba, na nakisi ya bajeti nchini Marekani.

    Bw. Lin amesema, Marekani kuongeza ushuru kwa bidhaa kutoka nchi za za nje ikiwemo China, Canada, nchi za Ulaya na Japan, hakusaidii kutatua suala la urari wa biashara, badala yake, ongezeko la ushuru limewalazimisha wateja wa nchi hiyo kulipa pesa nyingi zaidi wanaponunua bidhaa. Amesema,

    "Takwimu za mwaka jana zinaonesha kuwa, ingawa serikali ya Marekani imeongeza ushuru kwa kiasi kikubwa, lakini nakisi ya urari wa biashara ya Marekani na nje iliongezeka kwa asilimia 12.1. Hatua ya kuongeza ushuru haiwezi kutatua urari mbaya kwenye biashara. Badala yake, imeleta hali ya wasiwasi ya uhusiano wa biashara, na kusababisha hasara kwa wateja na kampuni za Marekani."

    Hivi sasa, China ni mwenzi mkubwa zaidi wa biashara wa nchi zaidi ya 120 duniani. Watalaamu wanasema, katika miaka ya hivi karibuni, uagizaji wa bidhaa kutoka nchi za nje umeongezeka kwa kasi kufuatia ongezeko la matumizi ya watu nchini China, na hali hii italeta fursa kubwa kwa nchi mbalimbali ikiwemo Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako