• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema majadiliano yawe na maana na uaminifu

    (GMT+08:00) 2019-05-23 19:27:02

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Bw. Lu Kang amesema China inatarajia Marekani itakuwa na mtazamo makini wa kurudi kwenye meza ya mazungumzo, na mlango wa China wa kufanya mazungumzo uko wazi, lakini majadiliano hayo yanatakiwa kuwa na maana na uaminifu.

    Bw. Lu amesema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya waziri wa fedha wa Marekani Bw. Steven Mnuchin kusema Marekani ina mtazamo wazi wa kufanya majadiliano ya raundi mpya na China na kutarajia pande hizo mbili zitarudi tena kwenye meza ya mazungumzo.

    Bw. Lu amesema Marekani inazishinikizia kampuni za sayansi za China kwa kutumia nguvu za taifa kwa malengo ya kisiasa, kitendo ambacho kinaathiri maendeleo na ushirikiano wa sayansi duniani, pia kinadhuru maslahi ya kampuni nyingi, hivyo haitapata uungaji mkono wa jumuiya ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako