• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Huawei yasaidia Uingereza kuzindua huduma ya kwanza ya 5G

  (GMT+08:00) 2019-05-23 19:27:27

  Kampuni ya mawasiliano ya simu nchini Uingereza EE, imetangaza kuwa itafungua huduma za teknolojia ya 5G katika miji sita mikubwa ya Uingereza mwishoni mwa mwezi huu, ambayo itakuwa ni mara ya kwanza kuzindua rasmi huduma ya 5G nchini Uingereza. Kampuni hiyo imesema itaendelea kutumia vifaa vya Huawei katika miundombinu kadhaa ya mtandao wa 5G.

  Kampuni ya EE imesema mtandao wa 5G unategemea mtandao wa 4G uliopo, watumiaji wanaochagua huduma mpya wataweza kupata mitandao ya 4G na 5G kwa wakati mmoja, hata katika maeneo yaliyojaa zaidi wanaweza kupata huduma nzuri zaidi. Kampuni nyingine ya Vodafone itazindua huduma ya 5G kuanzia mwanzoni mwa mwezi Julai katika miji saba ya Uingereza.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako