• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TPSF yasema sheria ya kodi inaathiri sekta binafsi

    (GMT+08:00) 2019-05-23 20:57:48

    Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Salum Shamte, amesema kuwa sekta binafsi nchini humo imeathirika kutokana na sheria ya kodi, viwango vya juu vya kodi na nguvu kubwa inayotumika katika zoezi la kukusanya kodi ,jambo lililosababisha biashara nyingi kufungwa.

    Shamte aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati wa ufunguzi wa mkutano wa majadiliano baina ya sekta binafsi kanda ya kati ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kutimiza miaka 20 ya taasisi hiyo.

    Alisema kuwa kulingana na ripoti iliyotolewa Waziri wa Viwanda na Biashara ni kwamba biashara zipatazo 16,000 zimefungwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

    Aidha, alisema kuwa Tanzania katika suala la mazingira ya uwekezaji na kufanya biashara imeendelea kushuka kutoka nafasi ya 137 ulimwenguni mwaka 2016 hadi nafasi ya 144 mwaka 2017 kama inavyoonyeshwa katika ripoti ya Benki ya Dunia ya urahisi wa kufanya biashara ya mwaka 2018.

    Wakati huohuo Shamte alimshukru Rais Magufuli na Waziri wa Fedha na Mipango kwa kulikemea suala hilo na kuongeza kuwa wamewasilisha mapendekezo yao serikalini ya namna ya kuboresha suala zima la kodi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako