• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Sevilla yatoka nyuma na kuipiga Simba 5-4, Bocco mchezaji bora wa mechi

  (GMT+08:00) 2019-05-24 09:27:52

  Mzoefu ni mzoefu tu ndivyo unavyoweza kusema, timu ya Sevilla ya Uhispania imefanikiwa kutwaa kombe la SportPesa Challenge baada ya kuwafunga wenyeji wao Simba ya Dar es Salaam mabao 5-4 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliopigwa usiku wa jana uwanja wa Taifa jijini Dar.

  Haukuwa ushindi mwepesi kwani Sevilla walilazimika kutoka nyuma kwa mabao 3-1 hadi mapumziko ili kushinda 5-4.

  Mara baada ya mchezo, nahodha wa Simba John Raphael Bocco alikabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa mechi. Zaidi ya watu nusu bilioni waliushuhudia mchezo huo mkubwa kuwahi kuchezwa Afrika Mashariki katika miaka ya hivi karibuni, ukiacha ule wa Gor Mahia dhidi ya Everton wa mwaka 2017

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako