• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shirika la umeme la Zimbabwe lalaani kuharibiwa kwa miundombinu wakati nchi hiyo ikikabiliwa na upungufu wa nishati

  (GMT+08:00) 2019-05-24 09:33:54

  Shirika la Kuzalisha na Ksambaza Umeme la Zimbabwe ZESA limesema, linahitaji dola milioni 15 za kimarekani kurekebisha miundombinu iliyoharibiwa, wakati nchi hiyo inakabiliana na msukosuko wa nishati unaolilazimisha kuwa na mgao wa umeme.

  Hivi karibuni Shirika hilo liliweka ratiba ya mgao wa umeme kwa nchi nzima kutokana na kupungua kwa uzalishaji wa umeme katika kituo cha uzalishaji wa umeme cha Kariba na ukosefu wa fedha za kigeni kununua vifaa kutoka nchi za nje.

  Wakati huohuo, uharibu wa makusudi pia umechangia upungufu wa nishati kwa baadhi ya wateja, wakati Shirika hilo likiendelea kupambana na tatizo hilo lililogharimu mamilioni ya dola katika matengenezo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako