• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasisitiza mafunzo zaidi kwa wafanyakazi

  (GMT+08:00) 2019-05-24 09:53:10

  Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amesisitiza mafunzo zaidi kwa wafanyakazi, ili kuwafanya wawe na elimu, ustadi na uvumbuzi.

  Bw. Li ameyasema hayo kwenye mkutano uliofanyika kwa njia ya simu kuhusu mafunzo ya ufundi stadi. Amesema uzinduzi wa mafunzo ya ufundi stadi ni hatua muhimu ya kuboresha uwezo wa watu wa kupata ajira na kuanzisha biashara, na kupunguza matatizo ya kimuundo ya ajira, na kuhimiza ajira. Ameongeza kuwa mafunzo hayo pia yataimarisha maendeleo ya kiuchumi yenye ubora wa hali ya juu.

  Aidha, Bw. Li amesisitiza matumizi mazuri ya mfuko wa bima ya ukosefu wa ajira wa dola bilioni 14.8 za kimarekani, na mifuko mingine kwa ajili ya mafunzo ya nguvukazi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako