• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wakuu wa majimbo ya Marekani wakosoa sera ya biashara ya nchi hiyo

  (GMT+08:00) 2019-05-24 10:25:54

  Wakati Marekani inapoongeza mvutano wa biashara na China, kongamano la 5 la wakuu wa majimbo ya China na Marekani linafanyika mjini Lexington, Marekani. Maofisa waandamizi wa majimbo ya Marekani wamesema sera ya biashara ya nchi hiyo imeleta utatanishi, na inaumiza kampuni za nchi hiyo.

  Mkuu wa jimbo la Kentucky la Marekani Bw. Matt Bevin amesema, kutokana na hali ya hivi sasa, utatanishi wa sera umeleta matatizo kwa uwekezaji wa kampuni za Marekani. Anasema,

  "Utatanishi utaleta usumbufu kwa kampuni za Marekani. Pia utaleta hasara kubwa, kwani licha ya hasara ya gharama, pia kuna hasara kubwa zaidi ya kukosa fursa."

  Kwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita, China na Marekani zimefanya duru nyingi za mazungumzo kuhusu suala la uchumi na biashara. Lakini mwanzoni mwa mwezi huu, Marekani ilitangaza ghafla kuongeza ushuru wa bidhaa kutoka China, na kuongeza hali ya wasiwasi ya uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili. Hivi karibuni baadhi ya vyombo vya habari vimesema uchumi wa China na Marekani unatengana. Bw. Bevin anasema,

  "Uchumi wa China na Marekani kamwe hauwezi kutengana. Kwa nini? Kwa sababu Marekani haiwezi kukosa China, na China pia haiwezi kukosa Marekani. Hii ni kweli. Wamarekani wanapenda kununua bidhaa za China, na Wachina pia wanapenda bidhaa na huduma za Marekani. Tunahitajiana. China yenye nguvu kubwa itanufaisha Marekani, na Marekani yenye nguvu kubwa pia inainufaisha China."

  Naibu mkuu wa jimbo la Washington la Marekani Bw. Cyrus Habib amesema, serikali za majimbo mengi zaidi ya Marekani zinapaswa kutambua umuhimu wa kuendeleza uhusiano wa uchumi na biashara na China, na yeye mwenyewe atahamasisha majimbo mengine kuimarisha uhusiano huo. Anasema,

  "Ukweli ni kwamba, jimbo la Washington ni mtangulizi katika kuendeleza uhusiano na China. Moja ya madhumuni yangu ya kuhudhuria kongamano hili ni kuhamasisha wajumbe wa majimbo mengine 18 ya Marekani kuona uzoefu wetu mzuri, na kuendeleza zaidi uhusiano na China katika sekta za uchumi, elimu, utamaduni na nyinginezo."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako