• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mashambulizi ya ndege za Marekani zasababisha vifo vya watu wawili kusini mwa Somalia

  (GMT+08:00) 2019-05-24 19:14:14

  Jeshi la Marekani limesema ndege za vikosi vyake maalum vimefanya shambulizi dhidi ya mtandao wa kundi la al-Shabaab kusini mwa Somalia na kuwaua wapiganaji wawili.

  Kamandi ya jeshi la Marekani barani Afrika AFRICOM inayosimamia vikosi vya Marekani barani Afrika, imesema kwenye taarifa yake kuwa shambulizi hilo limefanywa kwa ushirikiano na serikali ya Somalia karibu na mji wa Baled Amin kwenye mkoa wa Lower Shabelle.

  AFRICOM imesema kundi la Al Shabaab limekuwa likitumia maeneo ya vijijini ya Baled Amin kupanga mashambulizi dhidi ya vikosi vya Somalia. Tangu mwaka 2017, jeshi la Marekani limeimarisha mashambulizi ya ndege dhidi ya kundi la Al-Shabaab linalovilenga vikosi vya Umoja wa Afrika na Somalia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako