• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • AU kuzindua ukuta wa kumbukumbu ya mashujaa wa Tume za Misaada za Umoja wa Afrika katika siku ya Afrika

  (GMT+08:00) 2019-05-25 16:46:08

  Umoja wa Afrika jana ulitangaza kuwa utawapa heshima Waafrika waliopoteza maisha yao wakati wakihudumu kwenye Tume za Misaada za Umoja wa Afrika kwa kuzindua ukuta wa kumbukumbu ndani ya maeneo ya makao makuu ya umoja huo yaliyopo Addis Ababa Ethiopia.

  Kwenye taarifa iliyotolewa jana, nchi 55 wajumbe wa Umoja wa Afrika zimesema uzinduzi wa ukuta huo utakuwa ni ishara muhimu ya sherehe ya siku ya Afrika ya mwaka 2019 inayoadhimishwa leo Mei 25, siku ambayo Umoja wa nchi Huru za Afrika OAU ambao sasa ni Umoja wa Afrika, ulianzishwa mwaka 1963. Kwa mujibu wa AU ukuta wa kumbukumbu utazinduliwa ili kuwaheshimu mashujaa waliopoteza maisha yao kwenye Tume za Misaada za Umoja wa Afrika. Tume hizo ni pamoja na ya nchini Sudan AMIS, Kikosi Maalumu cha Kazi nchini Burundi AMIB, Tume ya AU nchini Somalia AMISOM, ya Mali AFISMA na ya Jamhuri ya Afrika ya Kati MISCA.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako